Mwafrika wa kwanza kufika mwezini afariki'

Raia wa Afrika Kusini aliyeshinda nafasi ya kuwa mwafrika wa kwanza kufika mwezini amefariki kwa ajali ya pikipiki kabla ya ndoto yake kuwa kweli.

Mandla Maseko, ambaye ni mwanachama wa kikosi cha anga nchini Afrika kusini, mwaka wa 2013, aliwapiku wengine milioni moja na kupata nafasi moja kati ya 23 katika chuo cha masuala ya anga nchini Marekani.

Alitumia juma moja akiwa katika kituo cha mafunzo cha Kennedy Space mjini Florida akifanya majaribio yakiwa ni maandalizi ya safari fupi ya anga ya muda wa saa moja , ambayo ilipangwa kufanyika mwaka 2015. Baadaye Kampuni iliyokuwa ikiratibu safari hiyo, XCOR Aerospace, ilifilisika mwaka 2017 na kusimamisha ndoto zake kwa muda.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad