Mwanajeshi mmoja nchini Gambia amekiri kuhusika katika mauaji ya wahamiaji wapatao 50 mnamo 2005 kutokana na agizo la rais Yahya Jammeh, anayearifiwa kuwa alihofia kwamba wanaume hao walikuwa na nia ya kumpindua.
Luteni Malick Jatta alikuwa anatoa ushahidi mbele ya tume ya ukweli na maridhiano TRRC inayochunguza maovu yaliotekelzwa chini ya utawala wa miaka 22 ya Jammeh.
Hapo awali alikiri kuhusika katika mauaji ya mwandishi Deyda Hydara mnamo 2004 kwa agizo la kiongozi huyo wa zamani Gambia.
Jammeh - ambaye sasa anaishi uhamishoni huko Guinea ya Ikweta - amekana kuhusuika katika vifo vya wahamaiji na mwandishi habari huyo.
Deyda Hydara alikuwa muasisi mwenza na mhariri msimamizi wa gazeti la The Point nchini humo.
Jatta alisema alilipwa $1,000 kutekeleza maujai hayo, licha ya kwamba ni mpaka siku ya pili ambapo aligundua kwamba alikuwa amemuua Hydara.
Jammeh alitorokea Guinea ya Ikweta mnamo 2017 baada ya kushindwa katika uchaguzi.
Gazeti la the Point, ambako Hydara alikuwa akifanya kazi kablaya kuuawa mnamo 2004, limeangazia kwamba imechukua miaka 15 kutambua nani aliyemuua mwandishi huyo.
Katika mtandao wake, gazeti hilo limeweka bango tangu wakati huo lililoambatana na swali, "Ni nani aliyemuua Deyda Hydara?".
Gazeti hilo halikutoa tamko jingine kuhusu taarifa hii ya sasa. Hydara aliwahi pia kulifanyia kazi shirika la habari la AFP na waandishi wasiokuwa na mipaka.
Mwanajeshi wa Zamani Gambia Asema Rais Yahya Jammeh Alimuamuru Kuua
0
July 24, 2019
Tags