Mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera anayeandikia magazeti ya ndani na nje ya Tanzania anadaiwa kukamatwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi.
Inadaiwa kuwa Erick Kabendera alichukuliwa kwa nguvu na watu kutoka kwake nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam eneo la Mbweni.
Kabendera ambaye anaandikia magazeti ya ndani na nje ya Tanzania, inaelezwa amechukuliwa Jumatatu na watu hao.
Baadhi ya vyombo vya habari nchini Tanzania likiwemo Gazeti la Mwananchi pamoja na televisheni ya mtandaoni Mtetezi TV vinadaiwa kuthibitisha taarifa ya kutoweka kwa Bwana Kabendera baada ya kuzungumza na ndugu jamaa na marafiki zake.
Uchumi wa Tanzania waanza 2019 kwa kuyumba
"Wachezaji PSG wana ubinafsi mkubwa"
Mwili wapatikana nyumbani kwa nyota wa Arsenal
''Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa ndugu, watu ambao walimkamata walikuwa sita na walijitambulisha lakini hawakutoa vitambulisho vyao. Watu hao walieleza kuwa wanampeleka mwandishi huyo kituo cha polisi Oysterbay''. Imesema taarifa ya Watetezi TV.
Kamati inayolinda waandishi wa habari barani Afrika (CPJ) kupitia ujumbe huu wa Twitter imesema inachunguza taarifa ya kukamwa kwa mwandishi wa habari za uchunguzi nchini Tanzania Erick Kabendera aliyechukuliwa kutoka nyumbani kwake na "watu wasiojulikana " na mahala aliko hakufahamaiki:
Mwandishi wa habari na mtetezi wa haki za binadamu Ansbert Ngurumo pia amezungumzia kuchukuliwa kwa Erick Kabendera kwenye ukurasa wake wa Twitter akisema Kabendera alimfahamisha mwenzake mmoja uwepo wa maafisa wengi wa usalama na watu wasiojulikana nyumbani kwake kabla ya kutoweka ambapo simu yake haikuweza kupatikana tena Jumatatu usiku:
Mmoja wa wana ndugu ambaye ameomba hifadhi ya jina lake amesema, "Kabendera amechukuliwa na watu sita ambao walifika nyumbani kwake na kuingia kwa nguvu wakiwa na gari aina ya Toyota Alphard." limeripoti gazeti la Mwananchi nchini humo.
Loy Kabendera ambaye ni mke wa Erick anadaiwa kulieleza gazeti la Mwananchi usiku wa Jumatatu kuwa , watu hao walifika nyumbani na kujitambulisha kwamba ni polisi lakini hawakuwa tayari kutoa vitambulisho na wakalazimisha kuingia ndani.
Mwandishi afunguka kilichomkimbiza Tanzania
Mwandishi wa Tanzania aliyetuzwa azungumza na BBC
Loy anadaiwa kusema kuwa walimchukua Erick kwa nguvu hali iliyowafanya baadhi ya majirani kufika kushuhudia tukio hilo na wale waliodiriki kupiga picha walinyang'anywa simu zao na askari hao.
Mtangazaji, mwandishi wa habari na mwanablogu nchini Tanzania, Millard Afrael Ayo, amesema kamanda wa jeshi la Polisi Kinondoni Mussa Taibu amemthibitishia kuwa jeshi la polisi linamshikilia Bwana Kabendera:
Ruka ujumbe wa Instagram wa millardayoMwisho wa ujumbe wa Instagram wa millardayo
Awali gazeti la Mwananchi liliripoti kuwa lilijaribu kuwawatafuta Kamanda wa Polisi Kinondoni, Dar es Salaam nchini Tanzania, Mussa Taibu pamoja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kuhusu taarifa za Kabendera na kwa pamoja wakasema kuwa hawana taarifa ya tukio hilo huku wakiahidi kufuatilia.
Mwandishi wa Habari Akamatwa na Watu Waliojitambulisha ni Polisi na Ajulikani Alipo
0
July 30, 2019
Tags