Mwili wapatikana nyumbani kwa kiungo wa kati wa Arsenal nchini Misri


Mwili wa mtu umepatikana nyumbani kwa kiungo wa kati wa Arsenal Mohamed Elneny nchini Misri.

Babake Elneny, Nasser aliupata mwili huo wakati alipotembelea nyumba hiyo mjini Mahalla al-Kubra , ambayo iko takriban kilomita 100 kaskazini mwa Cairo.

Kisa hicho kiliripotiwa kwa polisi, ambaye wanasema mtu huyo alikuwa akijaribu kuiba nyaya za umeme.

Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 29.07.2019
Taifa Stars yaizuia Harambee Stars Tanzania CHAN
Real Madrid yasitisha uhamisho wa Gareth Bale
Inaaminika kwamba alichomwa na umeme wakati wa wizi huo. Nyumba hiyo ni mali mpya ambayo ilitolewa na familia ya Elneny kutumika kama ofisi.

Elneny ambaye amerudi Arsenal baada ya kuichezea Misri katika kombe la mataifa ya Afcon , aliambiwa kuhusu kisa hicho kupitia simu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad