Naibu Spika Tulia Afunguka "Tunashangaaa Sana Wanaombeza Rais Magufuli"



Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson amemsifu Rais John Magufuli na kusema kuwa chombo hicho cha kutunga sheria kinamuelewa sana  kutokana na kiu na juhudi zake kubwa anazoendelea kufanya katika utekelezaji wa miradi mikubwa nchini.

Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika maradi wa kufua umeme wa Rufiji mkoani pwani jana, Dk Tulia amesema si bunge tu basli pia wananchi wamekuwa wakimpa pongezi sana kutokana na utendaji wake mahiri.

“Huu ni moja ya miradi mikubwa uliyoanzisha sisi Bunge tumekuelewa na wananchi pia tunaowawakilisha wamekuelewa, jambo ambalo Bunge tunafurahi tunaposema ndiyo kule bungeni mambo tunaona yanatokea.”

“Zaidi ya Sh1 trilioni zimeshaingia, waliosema ndiyo wamefanikisha mradi huu, mawaziri wapo na wao huwa wanasema ndiyo, wanafanya kazi nzuri na wanawatumikia vizuri Watanzania, wapo wanaosema hapana wapo hapa lakini hata wao wanakuunga mkono kwa sababu ni sehemu ya bunge,” amesema Dk Tulia.

Amesema Bunge linaubeba uchumi wa viwanda kwa juhudi kubwa, “Tunashangaa wanaobeza, tunatazama treni, uchumi wa viwanda, wenyeviti wa kamati wapo hapa na watapeleka taarifa namna miradi hii yote inakusudia kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa kati na hakuna mradi ambao umesimama peke yake watakuelewa tu, bunge limekuelewa.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad