NANI AJUAYE KESHO?
Mwaka 2005 Diamond alisafiri kwenda Tanga kuomba kuperform kwenye show ya Q-Chilla. Mabaunsa wakamtimua. Alipojaribu kuwaelewesha wakambeba juu juu na kumchania Tshirt na kumtupa nje. Bahati nzuri Q-Chilla alijulishwa kuhusu purukushani hizo, na alipoenda akasema aruhusiwe kuingia na apewe nafasi ya kuperform. Leo wale mabaunsa pengine wanatamani kuwa mabaunsa wa Diamond lakini haiwezekani.
Joseph Kabila aliwahi kuelezea kuwa kipindi anaishi Tanzania aliwahi kushushwa kwenye basi porini huko mkoani Iringa kwa sababu hakuwa na nauli ya kutosha. Alijaribu kumuomba konda amshushe angalau mahali penye mji lakini hakumuelewa. Akamtelekeza porini. Akatembea kwa mguu hadi Nyololo ndipo akapata msaada. Leo yule konda pengine anatamani kupata nafasi walau ya kumuomba msamaha Kabila lakini haiwezekani. Hakujua kama aliyemshusha porini angekuja kuwa Rais wa nchi.
Mwanzoni mwa miaka ya 1980's Meneja wa hoteli moja ya kitalii huko Hangzhou, alimnyima kazi Jack Ma. Baadaye Jack Ma alianzisha kampuni ya Alibaba na kumuajiri mtu huyo aliyemnyima kazi kuwa Meneja masoko wa online auction hosting ya Alibaba.Donald Trump aliwahi kuajiriwa na Mike Tyson miaka ya 80,kama mshauri wake wa fedha,ila leo Trump ni Rais wa USA.isitoshe Tyson anatamani Trump ampe ajira.
Maisha ni kama sarafu iliyotupwa angani, huwezi kutabiri itadondokea upande upi. Hakuna anayedumu kwenye madaraka milele. Hakuna anayekuwa tajiri milele. Hakuna anayekuwa maskini milele. Vyote hivi ni vya muda tu. Ni suala la majira na nyakati.
*Mtu unayemdhihaki leo na kumuona sawa na takataka, inawezekana ndiye atakayeamua hatma ya maisha yako kesho*. Hakuna ajuaye kesho. Mheshimu kila mtu bila kujalisha yupo katika hali gani leo kwa sababu huwezi jua kesho atakuwa wapi. Mtumishi wako wa leo anaweza kuwa boss wako wa kesho, kwa sababu kwenye maisha hakuna kinachodumu milele.
Tumia nguvu zako, utajiri wako na mamlaka yako kwa hekima ukijua kuna kesho. Siku zote simamia haki. Usimdhulumu mtu, usimnyanyase wala kumkandamiza mwenzio kwa sababu tu ya mali, nguvu au madaraka uliyonayo.
Nani Ajuaye Kesho..? Soma Visa Hivi Ikiwemo cha Diamond Platnumz Kutupwa Nje ya Ukumbi Show ya Q Chilla Tanga Mwaka 2005 Alipoomba Kuperfom
0
July 25, 2019