Nape Nnauy:" Wakubwa Wananichukia Wacha Wanichukie Napigania Haki za Wananchi"



Mbunge wa jimbo la Mtama (CCM), Nape Nnauye amesema hana kinyonga na serikali yake na kwamba anapigania haki ya wananchi wake kama walivyoahidi kuwasimamia.

Nape alisema awali mbaazi ilikuwa inafanya vizuri sokoni baadaye ikashuka kutoka Sh 2000 hadi Sh 100.



“Ndio maana mbunge wenu nikawa mkali bungeni wapo watu wanasema Nape mkali na wakati mwingine wakubwa wanachukia lakini ninasema bora nichukiwe lakini watu wangu waone nimesimamia haki yao

Aliongezea kuwa:” CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi sina jambo baya na mtu sina kinyongo na serikali yangu lakini tuliwaahidi tutasimamia haki yenu wanaosema Nape anaisemea Kusini yote ndio ni kweli Kusini yote ni maskini.

Nape alisema anatambua nia ya Rais John Magufuli alitaka kuwaokoa kutoka katika bei mbaya akapanga mpango bahati mbaya waliomshauri na waliotekeleza wakalikoroga.

“Nilivyokuwa nawaambia nyie mnamkorogea Rais waliniona mimi ni mbaya haiwezekani maoni yangu inawezekana waliolipwa wengi ni Kangomba kuliko wananchi wa kawaida sasa tumemkimbia nani hiyo milima na mabonde iliyotokea imetufanya wote tujifunze ndio maana juzi bungeni nikaiomba serikali tupitie upya sheria ya korosho,”. alisema Nape.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nabee usijitoe Kimasomaso...!!!
    Garasa lako ulidhani ni Joker limefichuka .

    Hata kwa mrisi..hamtotoka NIKAPA TUUU.

    JITATHMINI KALA HAUJA UMBUKA.

    ReplyDelete
  2. Nabee usijitoe Kimasomaso...!!!
    Garasa lako ulidhani ni Joker limefichuka .

    Hata kwa mrisi..hamtotoka NIKAPA TUUU.

    JITATHMINI KALA HAUJA UMBUKA.

    ReplyDelete
  3. Umesha Rudishaa Kadi ya Chama...!!!
    Au unangoja uaambiwe baada kikao cha
    kamati..USIJICHELEWESHE UKA UMMBUKA.

    Wala usione haya..ussipo kidhi Ahadi za chamasi huwa unakosaga sifa za kuendelea kuwepo Chamani..!!! Au nakoseaga. Pole pole unatafuta Ustaarabu mwingine.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad