Nawaambia zaeni tu, ndio maana uchumi wa China upo juu - Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kadiri idadi ya Watanzania inavyoongezeka ndivyo na uchumi nao unakua.

Ameyasema hayo leo wakati akizindua Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato iliyotokana na kuunganishwa kwa Mapori ya Akiba matatu ambayo ni Burigi, Biharamulo na Kimisi katika Mikoa ya Geita na Kagera.

"Nawaambia zaeni tu,ukishakuwa na idadi kubwa umetengeneza uchumi ndio maana uchumi wa China upo juu kutokana na population,najua nikizungumza hili wale watu ambao wamezoea kubania mayai watalalamika sana, nyinyi yaachieni waacheni wayabanie ya kwao" amesema Rais Magufuli.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amesema, “Idadi ya tembo imeongezeka kutoka 43330 mwaka 2016 hadi kufikia zaidi ya 60000 pia faru wameongezeka kufikia 163 hivyo hatuna budi kumpongeza Faru Rajabu (mtoto wa faru John) ambae ameshazalisha watoto 40 nadhani yule wajina wangu alikuwa hajitumi vizuri".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad