Ndege ya Kijeshi Yaangukia Nyumba na Kuwaua Watu 18

Takriban watu 18 wamefariki na wengine kujeruhiwa baada ya ndege ndogo ya kijeshi kuanguka katika makaazi karibu na mji wa rawalpindi nchini pakistan.

Wafanyakazi watano na raia 13 walikuwa miongoni mwa waliofariki , kulingana na vyombo vya waokoji .

Ndege hiyo ilikuwa ikifanya mazoezi wakati ilipoanguka na kusababisha moto mkubwa katika nyumba kadhaa.


Shahidi mmoja alisema kuwa ndege hiyo ilikuwa imeshika moto kabla ya kuanguka. Ndege hiyo ya King Air 350 Turboprop ilidaiwa kupiga kona kabla ya kuwasili ilipokuwa ikielekea na baadaye kuanguka.


Rawalpindi, karibu na mji mkuju wa Islamabad ndio eneo la makao makuu ya jeshi la Pakistan na ndege hiyo inamilikiwa na kitengo cha mafunzo ya angani cha jeshi la Pakistan.

Waziri mkuu wa Pakistan Imran Khan alituma risala zake za rambirambi na kuwaombea kupona kwa haraka waliopata majerahai kulingana na ujumbe wa twitter uliotumwa na serikali ya Pakistan.

Je ndege hiyo ilianguka vipi?
Mashahidi katika eneo la mkasa wamesema kwamba ndege hiyo ilianguka katika nyumba ya familia moja katika makaazi.

''Nilikuwa macho wakati ndege ilipopita mbele ya chumba changu na tayari ilikuwa imeshika moto ikiwa hewani'', alisema mkazi Ghulam Khan''.

''Sauti yake ilikuwa inaogopesha na ilikuwa ndege ndogo. Ilianguka juu ya nyumba ambapo familia moja ilikuwa ikiishi''.

Shahidi mwengine , Yasir Baloch, alisema: Mkia wa ndege hiyo ulikuwa umewaka moto na ilichukua chini ya sekunde tatu kabla ya kuanguka kando ya nyumba yangu na kuchomeka.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad