NEC Yatangaza Uchaguzi Jimbo la Tundu Lissu

NEC yatangaza uchaguzi Jimbo la Tundu Lissu
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza uchaguzi mdogo katika Jimbo la Singida Mashariki, mkoani Singida utakaofanyika Julai 31, mwaka huu.

Akitangaza hatua hiyo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,  Jaji Semistocles Kaijage amesema ratiba inatokana na barua ya Spika inayoeleza kuwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Tundu Lissu amepoteza sifa ya kuwa Mbunge kutokana na kushindwa kuwasilisha kwa Spika tamko la mali na madeni na kushindwa kuhudhuria mikutano saba mfululizo bila ruhusa ya Spika.

“Tumezingatia  matakwa ya kifungu cha 37 (1) (b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343, kutoa taarifa kwa umma kuhusu uwepo wa uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Singida Mashariki,” Jaji Kaijage

Jaji Kaijage amesema, fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kati ya Julai 13 hadi 18 mwaka huu, uteuzi wa wagombea utafanyika Julai  18, na kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia Julai 19 hadi 30 na siku ya uchaguzi itakuwa ni Julai 31, mwaka hu
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. WABUNGE KAMA LISSU WAKIPIGWA CHINI TANZANIA HATUNA HASARA BADALA YAKE TUNA FAIDA KUBWA KWA KUONGEZA KASI YA MAENDELEO YA NCHI.
    WATU KAMA YEYE NI MZIGO MKUBWA KWA TAIFA.
    UsirudieKosaKupigiaKuraUpinzaniOvyo!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad