Wakazi wa kata ya manda wameyasema hayo wakati wakizungumza na Muungwana blog mala baada ya timu ya waandishi wa habari kutoka chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe (NPC) kufika katika kata hiyo kwa ajili ya bonanza la michezo na hatua za awali kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika mkoa huo.
Clementine ngaile na Sophia chakwe ni miongoni mwa wananchi wa kata ya manda wanasema ufugaji wa aina hiyo umeanza mda mrefu huku sababu mojawapo ikiwa ni uhaba wa chakula lakini viongozi wamekuwa wakipiga marufuku uzululaji wa mifugo kama ng’ombe,nguruwe, mbuzi bila ya kupata mafanikio.
“ni kweli tupo kinyume cha sheria lakini tumezoea kuwafunga kamba mguuni jioni lakini asubuhi kuna wengine tuna waachia wanakwenda kutembea na nyumbani wanakuwa wanapafahamu watarudi hapa nyumbani wanakunywa maji halafu wanaendelea kutembea,kuna faida utakuta hakondi kwasababu anapata chakula lakini bado kuna wengine wakienda nyumba za jirani wanaharibu vitu wanapigwa mfano hawa wadogo utakuta wanakufa kwa kupigwa huku wengine wanavunjwa miguu,lakini ufugaji wa kwenye mabanda ni mzuri ila hatuna namna tutafanyaje tumeshazoea”alisema Sophia chakwe mkazi wa kata hiyo
Aidha wameongeza kuwa“unaona nguruwe wengine wale wako barabarani wanajitafutia chakula uongozi umelala kwasababu kama unafuga mifugo kama hii ulitakiwa uihudumie sasa watu wengine wanashindwa hata kulima bustani kwasababu kila aina ya mifugo ipo nje na kuna nguruwe wengine wanatafuna hata kuku”alisema mwananchi ambaye hakutaka kujitambulisha."
Kafisa mwambene ni afisa wa kilimo na mifugo kata ya manda,anasema wafugaji wa kata hiyo wamekuwa wakifuga kwa mazoea licha ya kuwa baadhi ya viongozi wanajitahidi kutoa maelekezo bila ya mafanikio na kutishiwa kulogwa.
“Viongozi tumekuwa tukijitahidi kuhimiza kufuga kisasa lakini wananchi wamekuwa wakisema mbona babu zetu walikuwa hivi sasa sisi tunawezaje kubadilisha mfumo,na matokeo yake imekuwa ni changamoto hata ushirikiano umekuwa mdogo na zaidi unakuta wengine wanatishia ushirikina ukikamata mifugo yake unatishiwa kulogwa mpaka inafika sehemu viongozi wengi kwa kuwa ni wa kuchaguliwa na ni wa maeneo ya huku wanaogopa kulogwa”alisema Mwambene
Mwambene amesema mara kwa mara mkuu wa wilaya ya Ludewa amekuwa akifika katika maeneo hayo kwa ajili ya kupiga marufuku lakini bado changamoto hiyo imekuwa ikiendelea kwa kuingiliwa na siasa.
“Mkuu wa wilaya amekuwa akitembelea kwenye kata hizi na amekuwa akiwaambia kinachotakiwa ni kufunga mifugo yenu lakini utekelezaji umekuwa ni kidogo kwasababu hata mambo ya kisiasa yanaingia kwa kuwa kata yetu ina mchanganyiko wa vyama vya siasa japo mpaka sasa tunazidi kutoa elimu huenda tukafanikiwa”aliongeza afisa kilimo na mifugo.