Nkamia: Kinana na Makamba Wamekengeuka Waombe Radhi



Mbunge jimbo la Chemba, Juma Nkamia, amesema Makatibu Wakuu wastafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) walioandika waraka wamekengeuka na wanatakiwa kuomba radhi.

Makatibu wastaafu hao ni Yusuph Makamba na Abdulrahman Kinana waliandika waraka huku wakilalamikia kutupiwa tuhuma zenye uongo na kuomba achukuliwe hatua Cyprian Musiba ambaye amekuwa akiwachafua kwa mambo ya uongo.

Nkamia amesema kinana na makamba wana nafasi ya kwenda kumuona Mwenyeketi wa chama na kumjulisha hayo malalamiko kama kweli yapo bila hata ya kuandika waraka.

‘Ikifika hatua makatibu wastaafu badala ya kufuata utaratibu wa chama wao wanaenda kuandika kwenye mitandao sijui waandishi wa habari huko ni kungengeuka na chama chetu kina taratibu zake mambo mengi ya chama yanaamuliwa kwenye kikao,” alisema Nkamia.

Aliongezea kuwa:”Kama inafika hatua wanatoka nje maana yake ni kungeuka na hata hizo sauti hata mimi nimezisikiliza hivi kweli Rais wa nchi unaweza kumuambia ni mshamba amekuwa waziri kwa miaka 20 leo kumuita mshamba ni kungeuka ndio maana nilitoa mfano ukiwa unakunywa bia sasa umeacha bia ukaanza kunywa wazuki lazima utachanganyikiwa kidogo,” alisema Nkamia.

Nkamia alisema kazi ya mwenyekiti wa chama ni kutekeleza ilani ya chama na walioitengeneza ilani ni Katibu Mkuu Kinana na Rais ameingia kutekeleza ilani aliyoikuta.

Aidha, alisema kuna tatizo lipo sehemu na kilichojitokeza ni tamaa za vijana na tayari ya wengine wamebebwa kwa sababu ya baba zao na kuona kama chama ni cha kwao.

‘Nilizani mzee Makamba na Kinana wafike mahali waombe radhi wamekitumikia chama ikifika wakati wa kuanza kutukanana katika mitandao kama huyo Musiba anaona amekosea wangempeleka mahakamani,” alisema.

Alisema wasitumie wazazi wao kama kinga ya kuwafikisha wanakatoka kufika “Mimi nimejisimamia mwenye baba yangu hakuwahi kuwa hata balozi wa nyumba kumi na kama taifa tuyakemee na wale waliokengeuka
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad