Pedi za Kiume zaingia Nchini..Hawa Ndio Wanaume Watakao Zitumia


Imezoeleka kuona au kusikia kwamba pedi zinatumiwa na watu wa jinsi ya kike, yaani kina mama pamoja na kina dada kutokana na uhitaji wao katika kujisitiri wakati wakiwa katika siku zao za mzunguko wa mwezi.

Lakini kuna habari ya kushangaza kidogo kutoka kwa kampuni mojawapo hapa nchini inayojihusisha na masuala ya ujasiriamali wa bidhaa mbalimbali.

Kampuni hiyo imetambulisha bidhaa mpya kabisa nchini, bidhaa ambayo ni pedi kwaajili ya watu wa jinsia ya kiume au wanaume kwa jumla.



Pedi hizo za kiume hutumika hususan kwa wanaume ambao wanasumbuliwa na matatizo ya tezi dume, ambapo wanakuwa wakivaa ndani ya nguo zao za ndani.

Matumizi ya pedi hizo ni kama yale ya kawaida, kwa maana kwamba mtumiaji akishaitumia basi hutakiwa kuitupa.

Angalia video kupata uelewa zaidi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad