Pole Pole Atoa Mpya "Sijaona Wala Kusikia Malalamiko ya Akina Kinana"
2
July 22, 2019
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema hajaiona nakala ya barua ya malalamiko ya kudhalilishwa iliyowasilishwa na makatibu wakuu wawili wastaafu wa chama hicho, Yusuf Makamba na Abdulrahman Kinana.
Polepole Jumapili kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kupitia mtandao wa WhatsApp kuwa hajasikia malalamiko hayo kwa kuwa kwa sasa yupo kwenye ziara vijijini.
Wakati Polepole akisema hajasikia malalamiko hayo ambayo si tu yameandikwa na vyombo vya habari, waraka wake pia umesambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwamo WhatsApp na hivyo kuzua mjadala mkubwa kabla na baada ya baadhi ya wabunge wa chama hicho kuendelea kujitokeza kila siku kuwajibu wastaafu hao.
Polepole ambaye alitafutwa na gazeti hili kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa CCM kuhusu barua hizo na hatua ambazo itachukua dhidi ya malalamiko ya viongozi hao wastaafu wa chama hicho, alisisitiza kuwa atakapoiona atatujuza.
Jumapili iliyopita Makamba na Kinana walimwandikia barua Katibu wa baraza la ushauri la viongozi wakuu wastaafu wa CCM, Pius Msekwa wakilalamika kudhalilishwa kwa mambo ya uzushi na uongo na mtu anayejitambulisha kama mwanaharakati na mtetezi wa serikali na kushangaa chama hicho kukaa kimya
Tags
Siyo yeye tu..
ReplyDeleteHATA MIMI PIA.
Huu ni mchezo wa shinikizo la Kinana na Sijui kama kweli alikuwaga mtoto wa halali wa jWuye .makmba aliyeoombwa apotee anasikishwa Kamba tu.
Sidhani kama anajua mchongo wote na kinacho endelea.
Na kadi itapotezwa/ kusitishwa uanachama na hatimae kpoteza uwakilshi wwa wananchi kupigwa Mtama. na Nongwa zenu zisizo na kichwa na kuunda magenge na vikundi.
Ala kwani mwaharakati Musiba.
ReplyDeleteAnahuusishwaje na CCM..???
Kweli ndiyo maana Ukawekwa umuri Wa KUSTAAFU.
AKILI NI KWABAZIMECHOKAA NA ZINAHITAJI MAPUMZIKO NA UKIZINGANGANIZA NDIYO ZNALETA UPUUZI KAMA HUU.
HAWA VIJANA WA ZAMANI WAMESHA CHOKA NA AKILI PIA.