Profesa Kabudi Akanusha "Sijathibitisha Kama Azory Gwanda Amekufa"

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amekanusha kuwa amethibitisha 'kifo' cha mwanahabari Azory Gwanda.

Msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania, Dkt Hassan Abbas amemnukuu Proefa Kabudi kwa kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter akisema: "Nimepokea kwa masikitiko taarifa potofu zinazoendelea kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii ikinukuu kimakosa mahojiano yangu kwenye kipindi cha BBC FOCUS ON AFRICA zikidai kuwa nimethibitisha kwamba mwanahabari Azory Gwanda amefariki dunia."

Lakini Prof Kabudi pia amesema bado haijulikani kama Bw Gwanda yungali hai: "Mpaka sasa hakuna uthibitisho kuwa Azory yuko hai au amefariki. Vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuchunguza tukio hilo na matukio mengine yaliyotokea katika machafuko ya Kibiti, Pwani yaliyosababisha ama watu kadhaa kupoteza maisha au kupotea."

Makampuni ya kubeti matatani
Boti za Iran zaitia tumbo joto Uingereza
Kabudi amesema kuwa, kilichotokea ni tafsiri potofu ya kile alishokisema: "Hii sio tafsiri sahihi kuhusu kile nilichokisema. Katika mahojiano hayo nilieleza kuwa tukio lililotokea Kibiti lilikuwa ni la kuhuzunisha na wapo watanzania waliouwawa na wengine kupotea. SIKUTHIBITISHA kuwa Azory Gwanda amefariki."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad