Raia wa Kigeni Watatu Wakamatwa Wakisafirisha Dhahabu

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu watatu raia wa kigeni kwa kosa la kusafirisha madini aina ya dhahabu bila kuwa na kibali.  Watuhumiwa hao walikuwa wakitokea Wilaya ya Chunya kuelekea Jijini DSM.

Watuhumiwa hao ni Clive Rooney raia wa nchi  ya Ireland Ross Stephen Chertsey ,  raia wa Uingereza  pamoja na Robert Charles , raia wa Uingereza.

Tukio hilo lilitokea  July 3, 2019 uwanja wa ndege wa Songwe,  Watuhumiwa hao walikamatwa na maafisa wa usalama wa uwanja huo wa Songwe.

Madini hayo yalikuwa na uzito wa gramu 1,044.95.  Ufuatiliaji unaendelea kufanywa na Kikosi kazi cha kamati ya usalama  ya Mkoa. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad