Rais Magufuli aeleza upungufu uliokuwepo Wizara ya January Makamba


Hii leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amuapisha Mhe. George Boniface Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira na kuchukua nafasi ya January Yusuf Makamba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Katika hafla hiyo ya uapisho Rais Magufuli ameeleza mambo kadhaa ambayo hayakuwa sawa kwenye Wizara hiyo.

"Nakumbuka suala la mifuko ya plastiki lilichukua muda mrefu karibia miaka minne, nikasaini
halikutekelezwa, Makamu wa Rais akazungumza wee halikutekelezwa, Waziri Mkuu akaenda akazungumza Bungeni halikutekelezwa, mpaka mwishoni nilipotoa amri ya lazima ndio likatekelezwa" amesema.

"Kuna idara ya mazingira fedha nyingi zinatolewa na Wafadhili lakini haziwi reflected na miradi husika, Kuna miradi mingine ilikuwa miradi hewa kule Rufiji ikapandwa mikoko, mikoko kule haipo, Mh. Simbachawene nataka haya ukayashughulikie" ameeleza.

Ameendelea kwa kusema, ""Pasiwe na ucheleweshaji wa kutoa vibali vya NEMC kwa viwanda vyetu, sisi tunataka kuwa na viwanda vya kutosha na Wawekezaji wasiwekewe vipingamizi kwa visingizio vya NEMC, vibali hivi vitoke, ikiwezekana wawekeze kwanza vibali vya NEMC vitakuja baadae".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad