Hayo yamesemwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka, wakati akizungumza na waandishi habari kuhusu maonesho hayo ya Nanenane yanatarajia kuanza 1/8/2019 hadi 8/9/2019.
RC Mtaka amesema katika maonesho hayo yanatafunguliwa na Makamu Samia Suluhu na kauli mbiu yake ni Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa uchumi kwa wananchi na yanatarajia kuwashirikisha watu mbali mbali na yana lengo la kuwainua wakulima, viwanda na wajasiliamiali mbalimbali.
RC Mtaka amesema katika maonesho hayo wanatarajia kuwashirikisha watu zaidi ya elfu 50 ambapo pia yatawashirikisha maofisa mbalimbali wa Serikali ambao watakuwa na shughuli za kuwasaidia wananchi huku akiwataka wakulima na wajasiriamali kujitokeza kwa wingi katika maonesho haya.
Kwa upande wake Kaimu Afisa Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA) Emmanuel Kakwezi, amesema katika maonesho hayo BRELA watatoa huduma.
Kakwezi amewataka wananchi kujitokeza ili waweze kusajili biashara zao kwa urahisi katika msimu huu.