RC Kuwaweka Kitimoto DC Sabaya na Wafanyabiashara


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira, amesema amekutana na Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na kumsikiliza dhidi ya shutma zilizotolewa na mfanyabiashara kuwa amemuomba rushwa ya shilingi milioni 5, ambapo Mghwira amewataka viongozi wabadilike.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya.

Mghwira amesema kumekuwepo na malalamiko mbalimbali ya wafanyabiashara dhidi ya watendaji tofauti tofauti wa serikali, kutoka katika idara mbalimbalimbali hali inayoashiria ukwamishaji wa masuala ya biashara kwa nchi.

''Nimemsikiliza DC yeye kama yeye sasa itabidi tuwaite wote kwa vile wafanyabiashara wamelalamika hadharani na imebidi na sisi kamati ya usalama ya Mkoa tuwaite tuwasikilize ili watueleze kama kuna kero zingine tuzipunguze'' amesema Mghwira.

Julai 22 katika mkutano wa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro na wafanyabiashara wa mkoa huo, mfanyabiashara huyo alidai kwamba DC Sabaya alimpa vitisho na kutaka ampe rushwa ya kiasi cha shilingi milioni 5. Baadaye Sabaya alizijibu shutma hizo kwa kusema si kweli.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad