Sakata la Kuwamwagia Pesa Waandishi wa Habari Basata Wamuita Uwoya na Steve Nyerere


Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza amesema kuwa wameamua kumuita msanii wa filamu nchini, Irene Uwoya pamoja na Steve Nyerere, kufuatia kitendo alichokifanya Irene cha kuwarushia pesa waandishi wahabari katika mkutano wa wasanii, uliofanyika Julai 15, Dar

Akizungumza leo Julai 17, Mngereza amesema kufuatia wito huo, wao kama Baraza hawajapanga kuwachukulia hatua zozote zile za kisheria.

''Wajibu wa baraza ni kukaa na wasanii, halafu kuzungumza nao, na  baraza linafanya kazi kwa mujibu wa sheria lililoziweka na kama uliona yale ni masuala ya fedha", amesema Mngereza.

Aidha kwa upande wake Steve Nyerere amekiri kupokea taarifa hizo na kwamba yeye kama msanii na BASATA ni Serikali, hivyo atafika kama alivyotakiwa.

Aidha Steve alipoulizwa kuhusu kitendo cha Irene Uwoya kuwatupia waandishi wa habari pesa, amejibu ''No Comment"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad