Serikali kujenga uwanja mkubwa wa mpira Chato

Serikali imetangaza kujenga uwanja mkubwa wa mpira wilayani Chato, mkoani Geita ili kukuza sekta ya michezo nchini na kuvutia watalii na wawekezaji.

Uwanja huo unatarajiwa kuwa wa pili kwa ukubwa baada ya wa Benjamin Mkapa ulipo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati Medard Kalemani amesema hayo wakati akihutubia sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya taifa ya Burigi-Chato na kueleza kwamba uwanja huo utaitwa Chato Stadium na ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

"Hivi karibuni tunajenga Uwanja wa mipra Chato Stadium ambao utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya nchi yetu" amesema Waziri Medard Kalemani.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwani chato ina population kubwa? Si ni District tu? Sasa Nani atakwenda huko kuona mipira? Kwani watalii wanakuja kuona mipira au wanyama? Tafadhali msijenge Chato. Bali tafuteni kwenye ushawishi wa mashabiki wengi. Kwenye majiji. Chato hata hizo hotel za kutosha hao watazamaji wengi kwani zipo?. Tutumie pesa kwa mahesabu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad