Serikali ya kenya yaondoa vibali ya makampuni ya kubeti

Serikali ya Kenya imefuta kwa muda vibali vya makampuni takriban 27 ya mchezo wa bahati nasibu hadi yatakapolipa ushuru.

Hii inakuja karibu zaidi ya mwezi mmoja baada ya kikosi cha maafisa kutoka mashirika mbali mbali kufanya uchunguzi wa leseni za makampuni yote ya michezo ya bahati nasibu nchini Kenya.


Katika taarifa iliyotolewa Jumatano na Mkurugenzi wa Bodi ya Udhibiti na utoaji wa Leseni ya michezo ya Bahati nasibu nchini Kenya, Liti Wambua pia imeagiza makampuni yote ya simu za mkononi yenye huduma za huduma za kutuma na kupokea pesa kubatilisha nambari za makampuni hayo za pay bill zinazotumiwa na kampuni zilizoathiriwa na hatua hiyo.

Tayari wachezaji wa michezo ya bahati nasibu wameanza kupokea ujumbe unaoonyesha kuwa kuna tatizo kwenye mtandao wa mchezo mfano ni ujumbe huu:

Kamapuni ya mawasiliano ya simu za mkononi -Safaricom ambayo imekuwa ikitumiwa makampuni ya michezo ya bahati nasibu na kamari tangu yalipoanzisha michezo hiyo nchini Kenya, imesema kuwa agizo hilo la serikali ambalo litaathiri akaunti milioni 12 za kubeti , limeiacha njia panda kwasababu baadhi ya akaunti hizo zina pesa na makampuni kama vile SportPesa na Betin zimepata agizo la mahakama la kuendelea kufanya kazi.

Hata hivyo kupitia mawakili wa Safaricom pia imeomba iruhusiwe kubaki na alama za siri (codes) ili kuwaruhusu watu kutoa pesa zao kwenye simu za mkononi, na imeomba kutoa taarifa kwa umma juu ya uamuzi wa mahakama kuhusu leseni.

Ni kwanini vijana wanacheza kamari ?
Makampuni hayo ambao ni pamoja na SportPesa, Betin na Betway, pia yanakabiliwa na tisho la kushuhudia mameneja wake wa kigeni wa ngazi ya juu wakirudishwa makwao.

Makampuni ambayo tayari yamefutiwa vibali vya kufanyanyia kazi nchini Kenya ni pamoja, SportPesa, Betin, Betway, Betpawa, PremierBet, Lucky2u, 1xBet, MozzartBet, Dafabet, World Sports Betting, Atari Gaming, Palms Bet na Betboss miongoni mwa makampuni mengine.

Imeripotiwa kuwa makampuni hayo ya bahati nasibu yalishindwa kuthibitisha kuwa yanalipa ushuru kulinga na maagizo ya Bodi ya Udhibiti na utoaji wa wa michezo ya bahari nasibu- Betting Control and Licensing Board (BCLB).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad