Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu, baada ya shahidi kushindwa kufika mahakamani kwa muda mrefu.
Mrembo huyo wa Tanzania mwaka 2006 anakabiliwa na mashtaka ya kurekodi video ya ngono na kuisambaza katika mitandao ya kijamii.
Hakimu Mkazi Mkuu,Maira kasonde alimwachia huru mshtakiwa huyo chini ya kifungu cha 225(5) cha mwenendo wa mashtaka ya makosa ya jinai.
Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali,Gloria Mwenda kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Maira Kasonde kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili kusikilizwa lakini shahidi waliokuwa wakimtegemea wamepewa taarifa kuwa anaumwa.
Naye Wakili wa Utetezi,Albert Msando alidai kuwa taarifa iliyotolewa mahakamani hapo haijajitosheleza huyo ameanza kuumwa jana au juzi hivyo walitakiwa kutoa taarifa zinazojitosheleza inapotokea pale shauri linataka kuahirishwa.
“Pande zote mbili zinatakiwa kutoa taarifa zinazojitosheleza nakumbuka mahakama ilitoa agizo kama inapotokea mtu anaumwa anatakiwa apeleke hati inayothibitisha ndio kutokana na hilo ilimsababishia Wema kuwekwa rumande kwa wiki moja iweje huyo shahidi asifanyebkama mahakama inavyotaka,”alidai Msando.
Msando alidai mahakama hiyo ilitoa ahirisho ya mwisho katika shauri lililopita kwa upande wa mashtaka hadi sasa ni zaidi ya siku 60 mmekuwa mkiahirisha kutokana na shahidi kutokuwepo.
Alidai kuwa kutokana na suala hilo ameiomba mahakama hiyo isipokee maombi ya upande wa mashtaka la kuahirisha shauri hilo.
Hakimu Kasonde alisema mahakama ilikuwa tayari kusikiliza kwabushahidi tangu Machi28,2019 lakini ilishindikana kutokana kutokanabna shahidi kutokuwepo.
Kasonde alisema Aprili 18,2019 pia ilitakiwa isikilizwe lakini upande wa mashtaka hawakuleta mashahidi hadi leo hii upande wa mashtaka wamekuwa wakitoa sababu mbalimbali ikiwemo shahifi waliomuandaa ana udhuru au mgonjwa.
“Maofisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) ndiyo wsliobaini tukio hili na hawa wapo hapa jijini Dar es Salaam ndio waliotoabtaarifa polisi kwa nini wasije TCRA wa karibu mnataka mashahidi kutoka Arusha ,”alisema Masonde
Kasonde alisema kesi inapoamliwa kwa wakati inamfanya mshtakiwa afanye maendeleo yake ya kiuchumi ili aweze kupata kipato na taifa kwa ujumla
Baada ya maelezo hayo hakimu alisema anamuachia huru mshtakiwa chini ya kifungu cha 225(5) cha mwenendo wa mashtaka ya makosa ya jinai.