Simba Kumtanga Mchezaji Mpya Leo Ambaye Alikua Tegemezi Yanga

Baada ya kufanikisha kumrejesha mchezaji wake wa zamani Ibrahim Ajibu, kuna uwezekano mkubwa wa Simba SC kumtangaza beki Gadiel Michael ambaye ameshamaliza mkataba na Yanga.

Taarifa za ndani zinasema kuwa Michael ameshamalizana na Simba kwa kusaini mkataba wa miaka miwili tayari kuhudumu kwa misimu miwili ijayo akiwa na uzi mwekundu na mweupe.

Beki huyo ambaye ni sehemu ya nyota walioshiriki michuano ya AFCON na kikosi cha Taifa Stars kilichoondolewa kwa kuchapwa mabao 3-2 na Kenya, ameshindwa kuendelea na Yanga sababu ya kutoelewana juu ya dau la usajili.

Kushindwa kuelewana na Yanga imekuwa kama bahati pekee kwa watani zao wa jadi Simba kumalizana naye ambapo uwezekano wa leo majira ya saa saba za mchana kutangazwa upo.

Usajili wa Michael ndani ya Simba utakuwa ni wa pili kwa mchezaji aliyemaliza mkataba na Yanga katika msimu uliomalizika hivi karibuni (2018/19) kutua  Simba ikiwa ni baada ya Ajibu.

Ajibu alitangazwa na Simba wiki jana kwa kuingia mkataba wa miaka miwili na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara kwa misimu miwili ya mwisho mfululizo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad