Simba Yaachana na Emmanuel Okwi Mrithi Wake Kushushwa Hivi Karibuni

Inaelezwa kuwa ni rasmi Simba SC imeachana na mshambuliaji wake wa siku nyingi, Emmanuel Okwi na wekundu hao wamesema wanatarajia kushusha mrithi wake wakati wowote.

Mpaka sasa wachezaji waliopelekwa katika usajili wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ni 26 huku Mtendaji Mkuu Crescentius Magori akisema kazi imekwisha.

Magori alisema wamemaliza kazi kubwa na kilichobaki ni mchezaji mmoja ambaye ataziba nafasi ya Okwi na itakuwa ni ‘sapraizi’ kwa mashabiki wao.

Okwi ameamua kujiunga na Fujairah Football Club inayocheza ligi ya juu huko Uarabuni.

Hata hivyo, tayari Emmanuel Okwi ambaye amemaliza mkataba wake na klabu ya Simba, amevivutia vilabu mbalimbali vya Misri, Afrika Kusini, Saudi Arabia, Tunisia pamoja na klabu yake ya zamani Simba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad