Katika mwendelezo wa usajili kuelekea msimu wa 2019/20 klabu ya soka ya Simba imenasana saini ya mshambuliaji wa TP Mazembe, Deo Kanda.
Mshambuliaji huyo raia wa Congo DR, mwenye miaka 29 amejiunga na Simba leo kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Kanda amesaini mkataba wa mwaka mmoja kukipiga Msimbazi akitokea TP Mazembe, ambapo alikuwa mmoja wa wachezaji walioiwezesha timu hiyo kushinda ubingwa wa Afrika, mwaka 2009, 2010.
Kanda pia alifunga goli kwenye mchezo wa fainali ya klabu bingwa Afrika dhidi ya Esperance mwaka 2013.
Mshambuliaji huyo pia ameshiriki Kombe la Dunia la vilabu mwaka 2009, 2010, 2013. Mwaka 2010 walifika fainali na kufungwa 3-0 na Inter Milan.