Spika Mstaafu wa Bunge Pius Msekwa Aunga Mkono Tundu Lissu Kuvuliwa Ubunge

Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pius Msekwa amedai uamuzi uliofanywa  na Spika wa Bunge Job Ndugai wa kumvua Ubunge aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu uko sawa, kwani yeye alishawahi kuwavua Wabunge zaidi ya 50 katika kipindi chake, kwa kosa la utoro ndani ya Bunge.

"Uzoefu wangu mimi katika hili Spika yuko sawa kabisa, kwa sababu hata mimi mwenyewe nilishawavua Wabunge wengi kipindi cha uongozi wangu nawashangaa sana wanaohoji hatua hiyo, ni jambo la Kikatiba lililofanywa na Spika Ndugai" amesema Msekwa

"Mimi mwenyewe niliwavua wengi tu na wala sio mmoja, Wabunge wa Zanzibar walikiuka kifungu cha Katiba alichokinukuu Spika Ndugai, tena walikuwa kama 50 hivi wote nikawavua Ubunge na uchaguzi ulifanyikla tena." ameongeza Msekwa

"Inawezekana watu wakasema Tundu Lissu nchi nzima inajua kuwa anaumwa, lakini katiba haisemi kuwa lazima usikilize kutoka magazetini au mitandaoni inatakiwa Mbunge aandike barua." amesema Pius Msekwa

June 28 katika vikao vya kujadili miswada mbalimbali ya kisheria kwa ajili ya mwaka mpya wa fedha Spika Job Ndugai alitangaza kuwa jimbo la Singida Mashariki liko wazi kufuatia Mbunge wake kutotoa taarifa kuwa yuko wapi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad