Spika wa Bunge la Tunisia Mohamed Ennaceur, ameteuliwa kuwa Rais wa mpito wa nchi hiyo baada ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Beji Caid Essebsi, kuaga dunia mapema Alhamisi ya Julai 25.
Spika huyo wa Bunge anatarajiwa kuapishwa mapema siku ya Alhamis, ambapo Waziri Mkuu wa nchi ya Tunisia ametangaza siku saba za maombolezo.
Rais Essebsi amefariki akiwa na umri wa miaka 92 na kwamba amefariki akiwa hajamaliza muhula wake wa Urais.
Inaaminika kuwa Essebsi ndiye Rais mkongwe zaidi duniani ambapo aliingia madarakani baada ya kushinda uchaguzi huru wa kwanza wa nchi hiyo, kufuatia vuguvugu la maandamano katika mataifa ya kiarabu.