Sudan Yafunga Shule Baada ya Mauaji ya Wanafunzi Wanne

Mamia ya wanafunzi nchini Sudan wameandamana kukemea vitendo vya mauaji dhidi ya watu watano al-Obeid
Masomo nchini Sudan yameahirishwa kutokana na maandamano yaliyoibuka baada ya kuuawa kwa kupigwa risasi kwa watoto wa shule wakati wa mkutano.

Mamlaka ya utawala wa kijeshi umeamuru shule kufungwa nchi nzima kuanzia siku ya Jumatano.

Wanafunzi walikuanyika kwenye miji mbalimbali ikiwemo mji mkuu Khartoum baada ya raia kuuawa siku ya Jumatatu.

Watu watano walipoteza maisha katika jimbo la Kordofan, wanne kati yao ni wanafunzi.

Watu kadhaa walijeruhiwa baada ya wafyatua risasi na watu wengine wenye silaha kufyatua risasi wakati wa maandamano katika eneo la El-Obeid kuhusu mafuta na upungufu wa mkate.

Sudan kuwashtaki maafisa wa jeshi waliotekeleza uhalifu

Mamluki katili wanaotawala nchi kwa dhahabu

Kwa nini shule zimefungwa ?

Mamia ya watoto, wengi wakiwa kwenye sare za shule na kupunga bendera za Sudan, waliingia kwenye mitaa ya Khartoum siku ya Jumanne baada ya kuuawa kwa wenzao.

Maandamano ya wanafunzi yalifayika pia kwenye maeneo mengine ya mji mkuu na miji mingine.

Jumanne mamlaka ziliamuru kufungwa kwa shule zote nchi nzima.

''Amri zimetolewa kwa magavana wa majimbo yote kufunga shule za watoto wadogo, msingi, na sekondari kuanzia kesho(Jumatano) mpaka yatakapotolewa maelekezo mengine,'' shirika la habari la Suna limeripoti.

Kilitokea nini El-Obeid?

Video zilisambaa kutoa mji wa El-Obeid, Kordofan Kaskazini zilionyesha watoto wakiwa katika sare za shule wakiimba, lakini vilio vyao vya kutaka maisha bora vilinyamazishwa na milio mikubwa ya risasi.

Picha za kutoka hospitali zilionyesha watu wakiwa wametapakaa damu.

Madaktari wanaounga mkono waandamanaji wamesema, takribani watu 62 walijeruhiwa El-Obeid pia watu watano waliuawa.

Haki miliki ya pichaAFP
Image caption
Mauaji katika eneo la El-Obeid yalisababisha ghadhabu
Mamlaka zilitangaza hali ya tahadhari katika eneo hilo na muda maalumu wa kutembea barabarani.

Shirika la umoja wa mataifa linalohudumia watoto duniani, Unicef, limetaka mamlaka chini Sudan kufanya uchunguzi kuhusu mauaji yaliyotokea na kuhakikisha waliohusika wanafikishwa kwenye mikono ya sheria.

''Hakuna mtoto anayepaswa kuzikwa akiwa na sare za shule,'' ilieleza taarifa yao na kueongeza kuwa wanafunzi waliopoteza maisha al-Obeid walikuwa na umri kati ya miaka 15 na 17.

Mwenyekiti wa baraza la kijeshi nchini Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, amekemea mauaji hayo.

''Kilichotokea katika eneo la al-Obeid ni cha kuhuzunisha. Kitendo cha kuwaua raia waliokuwa wakiandamana kwa amani ni uhalifu ambao haukubaliki ambao unahitaji hatua za haraka kuchukulia,'' alinukuliwa na televisheni ya taifa hilo.

Mauaji katika eneo la El-Obeid yalitokea siku moja kabla ya viongozi wa maandamano kukutana na majenerali wanaoongoza Sudan, baada ya pande mbili kutia saini makubaliano ya kugawana madaraka mwanzoni mwa mwezi huu.

Viongozi wa maandamano waliahirisha mkutano huo baada ya mashambulizi yaliyotokea.

Makubaliano ya kugawana madaraka yaliyofikiwa tarehe 17 mwezi Julai, yanaeleza kuwa serikali mpya itakayoongoza itakuwa na viongozi wa juu wa kiraia sita na majenerali wa kijeshi watano.

Lakini ripoti iliyotolewa na tume ya uchunguzi iliyoundwa na jeshi kufanya uchunguzi kuhusu ghasia zilizojitokeza kwenye maandamano mjini Khartoum tarehe 3 mwezi Juni tayari ilishazua mtafaruku kabla ya matukio ya El-Obeid siku ya Jumatatu.

Viongozi wa maandamano hayo walipinga ripoti hiyo na ya baraza la kijeshiiliyosema watu 17 waliuawa mwezi Juni, wakati inadaiwa kuwa watu 87 waliuawa kati ya tarehe 3 na tarehe 10 mwezi Juni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad