Tafakuri ya Kigwangalla “Maisha ndiyo haya haya, hukuna mengine”


Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Nzega, Hamisi Kigwangalla amesema kuna watu Mwenyezi Mungu amewajaalia afya, elimu, familia lakini hawana furaha hata kidogo kwenye maisha yao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kigwangalla amesema kwamba watu hao wanadhani kwamba walivyonavyo havitoshi, wanaamini kwamba kuna kizuri zaidi mbele, na wanapaswa kuendelea kupambana kutafuta zaidi.

“Kuna watu tumejaaliwa na Mwenyezi Mungu afya, elimu, familia, mahala pa kulala, uhakika wa kula chakula kila siku na nguo nzuri za kuvaa, lakini hatuna furaha kabisa kwenye maisha yetu.”

“Tunadhani kwamba tulichonacho hakitoshi, wengi tunaamini kuna kizuri zaidi mbele, kwamba tuendelee kupambana kutafuta zaidi na zaidi. Kwamba hicho cha huko mbele ni kizuri zaidi na tukikipata basi ndiyo kitakacholeta furaha zaidi kwenye maisha yetu.”

“Sijui ni tamaa ama ni nini. Sijui ni ubinadamu wetu ama ni nini. Lakini hatujaridhika tu. Ni tamaa kama ya kuku, ambaye hata ukimmwagia mtama ama mchele hapo juu, badala ya kula ule anaoona, anazidi kuchakua chakua kwa nguvu zaidi akiamini pengine huko chini ndiyo kuna mwingine mwingi na mtamu zaidi.”

“Mara nyingi hujikuta akiufunika kwenye udongo na kupata taabu kuchakua na kuuona ili aweze kufaidi. Kuku angepaswa kujifunza kwa bata, yeye ukimtupia msosi huwa anakula anachokiona, hana muda wa kuhangaika kuchakua chakua kama kuku.”

Ameandika:
Kuna watu tumejaaliwa na Mwenyezi Mungu afya, elimu, familia, mahala pa kulala, uhakika wa kula chakula kila siku na nguo nzuri za kuvaa, lakini hatuna furaha kabisa kwenye maisha yetu. Tunadhani kwamba tulichonacho hakitoshi, wengi tunaamini kuna kizuri zaidi mbele, kwamba tuendelee kupambana kutafuta zaidi na zaidi. Kwamba hicho cha huko mbele ni kizuri zaidi na tukikipata basi ndiyo kitakacholeta furaha zaidi kwenye maisha yetu. Sijui ni tamaa ama ni nini. Sijui ni ubinadamu wetu ama ni nini. Lakini hatujaridhika tu. Ni tamaa kama ya kuku, ambaye hata ukimmwagia mtama ama mchele hapo juu, badala ya kula ule anaoona, anazidi kuchakua chakua kwa nguvu zaidi akiamini pengine huko chini ndiyo kuna mwingine mwingi na mtamu zaidi. Mara nyingi hujikuta akiufunika kwenye udongo na kupata taabu kuchakua na kuuona ili aweze kufaidi. Kuku angepaswa kujifunza kwa bata, yeye ukimtupia msosi huwa anakula anachokiona, hana muda wa kuhangaika kuchakua chakua kama kuku. Katika maisha yetu tujipe furaha pale tulipo. Shukuru kwa ulipo na hiyo iwe sababu yako ya kuwa na furaha. Furaha yako siyo matokeo ya mwisho ya jitihada unazofanya, bali ni sehemu ya mchakato wa maisha yako. Jipe furaha wakati wote wa mchakato. Maisha ndiyo haya haya, hukuna mengine. Endelea kupambana huku ukifurahia maisha. #NjeYaBox #HK #galla

A post shared by Dr. Hamisi Kigwangalla (@hamisi_kigwangalla) on Jul 27, 2019 at 6:29am PDT

“Katika maisha yetu tujipe furaha pale tulipo. Shukuru kwa ulipo na hiyo iwe sababu yako ya kuwa na furaha. Furaha yako siyo matokeo ya mwisho ya jitihada unazofanya, bali ni sehemu ya mchakato wa maisha yako. Jipe furaha wakati wote wa mchakato. Maisha ndiyo haya haya, hukuna mengine. Endelea kupambana huku ukifurahia maisha.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad