Taifa la Misri Latoa Agizo la Kusitishwa Mpango wa Kupiga Mnada Kichwa cha Mfalme Mdogo

Misri imetoa agizo kwa umba la kupiga mnada Christies kusitisha uuzaji wa mchongo wa kichwa cha mfalme mdogo Tutankhamun wenye umri wa miaka 3,000. Wizara ya mambo ya nje Misri inatuhumu kwamba mchngo huo huenda uliibiwa katika miaka ya 1970 kutoka hekalu moja. Mchongo huo wa inchi 11 ulitarajiwa kupigwa mnada leo London na unatarajiwa kugharimu zaidi ya $ milioni 5.


Kwa mujibu wa BBC. Christies inasema Misri haijaelezea wasiwasi kuhusu kichwa hicho katika siku za nyuma licha ya mchongo huo ‘kuonyeshwa wazi’.

Mchongo huo uliotengenezwa kwa jiwe gumu la madini ya quartz linatoka katika mkusanyiko binfasi wa sanaa ya jadi ambalo jumba hilo la mnada la Christie liliuza kwa pauni milioni 3 mnamo 2016.

Katika taarifa yake, Christies imesema: “Mchongo huo hauchunguzwi na haujawahi kuchunguzwa.”

Imesema haiwezi kupiga mnada kitu ambacho kinagubikwa na malalamiko ya halali.

Christies pia imechapisha mpangilio wa wamiliki wa mchongo huo katika miaka 50 iliyopita.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad