TAKUKURU yavisifu Vyombo vya Habari kwa Mapambano ya Rushwa


Vita ya Rushwa sio ya  ya Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Pekee bali ni jukumu la Kila mmoja wetu bila kujali jinsia,umri,dini wala kabila.

Katika kuhakikisha Wananchi wa mkoa wa Manyara wanapata Elimu ya mapambano ya adui huyo mkubwa anaepingwa vikali tangu enzi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na waasisi wengine wa Taifa hili la Tanzania,Kituo cha redio Smile Fm kinachorusha Matangazo yake kutoka mjini Babati kimeendelea kusambaza elimu  kupitia mawimbi huku ikitoa nafasi kwa wananchi kuuliza maswali kuhusu TAKUKURU na kujibiwa moja kwa moja na Maafisa wa Taasisi hiyo.

Hata hivyo TAKUKURU inakiri kwamba elimu hiyo kupitia kituo hicho cha Redio ya jamii  imeonekana kuzaa matunda kwa jamii ambapo wamekuwa wakipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi maeneo mbalimbali wakitoa taarifa Za vitendo ya Rushwa kupitia namba yao ya Bure ya 113.

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Fidelis  Kalungura ameupongeza Uongozi na watumishi wote wa Smile Fm Redio kwa mchango wao mkubwa katika Mapambano dhidi ya Rushwa kwa kusaidia kurusha hewani vipindi vya redio bila ya gharama zozote.

Kalungura anasema huo ni mfano mzuri wa Kuigwa na vyombo vyote vya habari  kwa kuzipa kipaumbele habari za Mapambano dhidi ya Rushwa ili kutoa hamasa kwa jamii na  kuunga Mkono mapambano dhidi ya Rushwa nchini yanayoongozwa na Dkt.John Pombe Joseph Magufuli,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha amewasihi wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa kwa njia ya Simu 113 au kutuma ujumbe kwa kubonyeza *113# pamoja na kufika ofisi za TAKUKURU katika wilaya na mkoa na sio kubaki kuwa watazamaji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad