TANAPA Yafungua Barabara Hifadhi Mpya Tatu

TANAPA Yafungua Barabara Hifadhi Mpya Tatu
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), limefungua Kilometa 248 za barabara katika hifadhi mpya za Burigi-Chato, Ibanda Kyerwa na Rumanyika-Karagwe.

Kufunguliwa kwa miundombinu hiyo kumetoa fursa pana kwa wawekezaji kutembelea maeneo ya uwezekaji yaliyoainishwa na TANAPA na kuwarahisishia watalii kutembea hifadhini.

Akielezea hatua zilizotekelezwa tangu hifadhi zitangazwe rasmi, Mhifadhi Mwandamizi Kitengo cha Ulinzi kwenye hifadhi hizo tatu, Upendo Massawe amesema  ufunguzi wa miundombinu zaidi unaendelea kufanywa.

“Kwa sasa hata mwekezaji akija anaweza kutembelea maeneo yaliyohifadhiwa na kuchagua angependa kuwekeza eneo gani.

“Hifadhi ya Burigi-Chato tumefungua Kilometa 218 na kwa Hifadhi ya Ibanda-Kyerwa na Rumanyika-Karagwe tumefungua Kilometa 30,” alisema.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu, amesema kazi kubwa ya kufungua barabara na viwanja vidogo vya ndege inaendelea.

“Kufungua miundombinu hasa Hifadhi ya Rumanyika-Karagwe na Ibanda-Kyerwa bado ni kazi kubwa, juhudi zinazofanywa sasa ni kuunganisha barabara zinazoanzia njia kuu  pamoja na zile za ndani,” amesema Kanyasu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad