Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Paramagamba Kabudi amesema kuwa Tanzania na Kenya ni ndugu wa damu.
Kabudi amesema kuwa mipaka ilipochorwa kuliibuka ubishani wa Ziwa Victoria, ambapo Wajerumani walitutawala, wakapewa 51%.
"Tanzania na Kenya ni ndugu wa damu, mipaka ilipochorwa kuliibuka ubishani wa Ziwa Victoria, Wajerumani walitutawala, wakapewa 51%, Balozi wa Ujerumani wakati huo, kupitia kitabu chake, alisema bila maamuzi hayo Nyerere angekuwa Mkenya si Mtanzania," amesema Kabudi.
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje Kenya, Monica Juma "Leo tuna furaha sana, nilikuwa kwa muda mrefu nikitamani kufika Dar, tumefika hapa leo kuleta ujumbe kutoka kwa ndugu yako Rais Kenyatta, amenituma kukuletea wewe ujumbe na pia dada na kaka zetu wa Tanzania kupitia wewe."
Kabudi ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati Rais Magufuli ameshuhudia makabidhiano ya dhahabu iliyokamatwa nchini Kenya yaliyowasilishwa na Mjumbe Maalum wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, makabidhiano hayo yanafanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.