Tapeli Mandazi Anayetumia Jina la Mh.Jokate Kutapeli Watu Mtandaoni Adakwa
1
July 25, 2019
Mheshimiwa Jokaye ameandika hayo hapo chini
"Kipekee naomba nimshukuru Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI) Robert Boaz kupitia Kitengo cha CYBER CRIME Kwa kufanikisha kumnasa mtuhumiwa wa utapeli ambae amekua akijipatia Fedha Kwa njia ya udanganyifu. Amefungua ukurasa Facebook Kwa Jina Langu na kudanganya watu kua ninatoa mikopo Kwa njia ya Saccos / Viccoba na hivyo wamtumie fedha Huyu Mtuhumiwa kwenye picha kupitia namba *0713924045* jina lake ni Abdalah Mbanjo ya kuomba mikopo na akiba ya asilimia kumi ya mikopo wanayoomba.
Kwa mara nyingine napenda kuijulisha jamii kwamba sina Taasisi yoyote ile inayotoa mikopo na watoe taarifa kituo chochote cha polisi iwapo mtu yoyote au taasisi yoyote itatumia jina langu au ofisi ya DC wa Kisarawe kujipatia fedha Kwa njia ya udanganyifu.
Baada ya mtuhumiwa huyu kutiwa nguvuni ilibainika kuwa yapo makundi mengine mengi ambayo yanatumia jina langu kujipatia fedha Kwa njia ya udanganyifu. Na yote tumeshafahamu yalipo. Nalishukuru Jeshi la Polisi Kwa kuwa wamejipanga kuwasaka popote walipo nchini na kuwafikisha kwenye Vyombo Vya Sheria.
Na wote wanaotumia jina langu vibaya kwenye mitandao tutawachukulia hatua kali. Mwisho ila sio kwa umuhimu Namshukuru na Kumpongeza IGP Sirro kwa kuwa na jeshi la polisi makini lenye kufanya kazi kwa weledi"
IGP Siro na Mr Boaz, mkamateni. Wingine kwenye Facebook, anatumia Jina na picha ya Janet Magufuli. Anasema anatoa mikono ya fedha
ReplyDelete