Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa awamu ya Nne, Bernard Membe, amesema sauti zilizovuja hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii ikihumusisha yeye akifanya mazungumzo na mtu asiyefahamika wakijadili juu ya sintofahamu ndani ya CCM ni ya kwake.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na vyombo habari, ambapo amesema kuwa ni kweli sauti iliyodukuliwa na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii ni ya kwake asilimia 100 huku akiomba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuingilia kati suala hilo.
“Sauti ni za kwangu ni mimi 100 kwa 100, na nimeifanyia kazi na ninajua imetoka wapi kwa sababu nina miiko ya kuzingatia sisemi, Ni sauti yangu kabisa na ninaelewa kila kilichotokea unaweza kuingia ugonjwa wa udukuzi, kama wale wanaotoa taarifa hizi za udukuzi hawachukuliwi hatua, wadukuzi wako duniani wanataka fedha tu,”amesema Membe.Read More:Nafasi za Ajira 291 Zilizotangazwa Leo
Hivi karibuni IGP Simon Sirro alisema kuwa wanafuatilia suala la sauti hizo na endapo wakigundua kuna kosa la jinai wahusika watafikishwa mahakamani.
Membe acha mchecheto. Hoja ni kwamba walidukua nini: usaliti, uhaini au ngono?! Yote mabaya lakini uzito unatofautiana.
ReplyDeleteUsirudieKosaKupigiaKuraUpinzaniOvyo!
Mjomba Membe...umeanza kuwa sijuu Jina au Sifa ipi nikupe..kwa Lugha nyepesi
ReplyDeleteniseme KICHEKESHO.
Hebu tujuze tena TATIZO NI NINI KATIKA UHAINI HUU.
W3WE UNGOJE ZAMA ZA NANIII AKIJA LADA AKUPE KAZI YA KULINDA GETI NA NCHALE.
NA HIYO NI BAADA YA BW DIWANI KURIDHIKA NA KIWANGO CHA PESA ZA NCHI
NA MISAADA ULIZO RUDISHA TOKA HUKO UGHAIBUNI...MBONA MTAUMBUKA SANA.
NA INJINIA WA MCHONGO WOTE NAWAPE WA MTAMA , ATI ANAZUNGUMZIA MBAAZI NA KOLOOSHO MSALITI HUYU.