Tatizo la Kijinsia Lazidi Kumuandama Semenya, Ashindwa Kutetea taji lake la ubingwa wa dunia

Caster Semenya anasema hatotetea taji lake la ubingwa wa mbio mita 800 duniani mwezi Septemba kufuatia uamuzi dhidi ya kesi aliyowasilisha mahakamani kuweka kuidhinisha viwango vya homoni ya testosterone miongoni mwa wanariadha wanawake.

Lakini mwanariadha huyo wa Afrika kusini amesema “ataendelea kupambana kutetea haki za binaadamu” licha ya “kuhuzunishwa kwake”.

Semenya amewahi mara mbili kukata rufaa dhii ya sheria za IAAF zinazomzuia kukimbia pasi kutumia dawa.

Lakini uamuzi unaomruhusu kukimbia sasa umebatilishwa.

Semenya anapinga sheria mpya za shirikisho hilo la riadha duniani IAAF zinazomtaka yeye na wanariadha wengine walio na utofuati wa ukuwaji kijinsia (DSD) lazima atumie dawa zinazopunguza homoni za testosterone ili kuweza kukimbia katika mbio za kuanzia mita 400 hadi maili moja au abadili mbio atakazoshiriki.

Semenya alikuwa anaweza kukimbia wakati kukisubiriwa uamuzi wa mahakama ya Uswizi, na akiwa awali alishindwa katika rufaa aliyowasilisha katika mahakama inayoshughulikia mizozo katika michezo (Cas) mnamo Mei.

Uamzui huu wa sasa wa mahakama ya juu zaidi ya Uswizi una maana kuwa hatoruhusiwa kushindana katika mashindano ya ubingwa duniani huko Doha.

“Nimesikitishwa sana kuzuia kulitetea taji langu nililioshinda kwa ugumu,” Semenya, mwenye umri wa miaka 28, amesema.

“Lakini hili halitonizuia kuendelea kupambana kutetea haki za binaadamu kwa wanariadha wote wanawake waliohusika.”

IAAF limesema linataka sheria hizo zilizosimamishwa ziidhinishwe kuepuka “mchanganyiko mkubwa” miongoni mwa wanariadha na waandalizi wa mashindano na “kulinda hadhi ya mchezo”.

Limnepinga tuhuma katika barua kwamba sheria zake “zinashinikiza ukosefu wa usawa wa kijinsia”, na kwa kujibu limeeleza kuwa sheria hiyo iliidhinishwa “mahsusi kwasababu IAAF inawajibika kulinda haki na fursa za wanariadha wanawake”.

Mnamo Mei, Semenya aliwasilisha rufaa katika mahakama hiyo baada ya kushindwa kushinikiza sheria hizo za IAAF kubatilishwa na Cas.

Dorothee Schramm, wakili aliyongoza rufaa ya Semenya aliongeza: “Uamuzi wa jaji hauna athari kwa rufaa yenyewe. Tutaendelea kuifukuzia rufaa ya Caster na kuzipigania haki zake msingi za binaadamu. Mashindano huamuliwa mwisho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad