Tido Mhando Azungumzia Mpango wa Kuileta Miili ya wafanyakazi 5 wa Azam Media

Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd, Tido Mhando amesema kuwa wanafanya mpango wa kuleta miili ya wafanyakazi hapa Makao Makuu yao Tabata.

Tido Mhando amesema hayo leo, huku akisema ni lini wataleta miili hiyo watatoa taarifa akiongeza kuwa maandalizi yote ya mazishi yanakwenda kulingana na taratibu na matakwa ya familia.

“Tunafanya mpango kwamba huenda tukawaleta wenzetu na kuwaaga makao makuu yetu hapa Tabata lakini lini tutafanya hivyo tutawaambia,” Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd, Tido Mhando.

“Tukio hili ni baya sana kuwahi kutokea na tuko karibu sana na familia kuhakikisha kwamba maandalizi yote ya mazishi yanakwenda kulingana na taratibu na matakwa ya familia,” amesema Tido Mhando.

Leo wafanyakazi watano wa Azam Media wamefariki leo Mkoani Singidakwenye ajali ya gari iliyotokea katikati ya Shelui na Igunga.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad