Tunda na Whozu mambo hadharani ‘Nimechagua love sio pesa

Stori kubwa ambayo imechukua headlines leo July 9,2019 ni kuhusu Mwanadada Tunda ambaye ame-post video kupitia ukurasa wake wa instagram ikimuonyesha akipigwa mabusu na mwimbaji wa Bongo Fleva Whozu na kuandika caption inayosema ‘Nmechagua LOVE sio PESA. This is new sweet Tunda’

Kupitia mahojiano tofauti aliyowahi kufanya Whozu alikuwa akikanusha taarifa zilizokuwa zikisambaa kuhusu ukaribu wake na Tunda na hata swali kuhusu kuwa na uhusiano wa kimapenzi lakini miezi kadhaa iliyopita Whozu alikiri kuwa aliwahi kushikiwa bastola na kunyolewa nywele kisa Tunda.



Inawezekana Tunda ameamua kuweka wazi kuhusu mahusiano yake na Whozu kupitia video pamoja na caption alizoziweka kwenye ukurasa wake wa instagram baada ya kuonekana kuficha swala hilo kwa muda mrefu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad