Aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amekiri kutomwandikia Spika Ndugai barua yoyote kuhusu mahali alipo wala hali yake ya kiafya.
Amesema si kwamba alisahau au alipuuza, bali ni kwa sababu Spika Ndugai alikuwa anafahamu fika mahali alipo na sababu za yeye kuwa huko
Wiki iliyopita Spika Ndugai alitangaza kumvua ubunge Lissu kwa kile alichoeleza kuwa kiongozi huyo hajulikana halipo zaidi ya kuonekana nchi za Ulaya na Marekani.
"Ni kweli sijawahi kumuandikia Spika Ndugai barua yoyote kuhusu mahali nilipo, na hali yangu ya kiafya. Sikumwandikia, sio kwa sababu nilisahau au nilipuuza, bali ni kwa sababu Spika Ndugai alikuwa anafahamu fika mahali nilipo, na sababu za mimi kuwa huko," amesema Tundu Lissu.
Ameendelea kwa kusema, "Kwa sheria na taratibu za Bunge, Spika na watendaji wake wanawajibika kufuatilia hali ya mbunge anayetibiwa nje ya nchi, na kutoa taarifa za maendeo yake. Sio wajibu wa mbunge mgonjwa kulitaarifu Bunge juu ya afya yake. Ndugai alipaswa kujua nilipo, na maendeleo yangu." Lissu,".
Aidha, Tundu Lissu amesema licha ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kudai hakujaza fomu za mali na madeni za viongozi wa Umma bado ana sifa za kugombea nafasi yoyote ya uongozi.
"Ili upoteze sifa ya kugombea ubunge au urais sharti uwe na hatia, sasa mimi sijakutwa na hatia na mahakama au mahakama ya Sekretarieti ya maadili, Ndugai peke yake hawezi kunitia hatiani bila kunisikiliza."
"Kwa hiyo mimi naweza kugombea nafasi yoyote ya uongozi iwe ubunge au urais. Kama wanataka nisigombee wanipeleke mahakamani au kwenye mahakama ya sekretarieti na wakiniuliza kwa nini sijajaza fomu nitawaambia nitawezaje kujaza nikiwa nje ya nchi," amesema Lissu
Amesema fomu hizo zinapaswa kujazwa na kuziwasilisha kwa njia ya mkono lakini zinapaswa kusainiwa na wakili wa Tanzania, "Sasa mimi niko hospitalini Ubelgiji, nawezaje kuzijaza, huku nampata wapi wakili, nawezaje kuzipeleka kwa mkono? Kwa hiyo walipaswa kuniuliza kwa nini sijajaza na si kuzungumza sijajaza bila kuwa na sababu."
Tundu Lissu Afunguka sababu ya kutomwandika barua spika wa Bunge, Job Ndugai
0
July 02, 2019
Tags