Tunisia kuomboleza kifo cha Rais wao kwa siku saba

 Kufuatia kifo cha Rais Beji Caid Essebsi siku ya Alhamisi (jana) asubuhi,Waziri Mkuu wa Tunisia Youssef Chahed aliamuru siku hiyo hiyo siku saba za kuomboleza ya kitaifa.

Serikali pia imeamua kufuta maonyesho yote ya kisanii na hafla zingine za kitamaduni nchini Tunisia,kulingana na taarifa iliyotolewa na urais wa serikali.

"Tunisia imempoteza raia mwaminifu, mwananchi aliyejitoa na maisha yake kwa hatua za kitaifa," Waziri mkuu wa Tunisia aliandika kwenye akaunti yake rasmi ya mtandao wa Facebook.

Rais Essebsi aliaga dunia siku ya Alhamisi (jana) akiwa na umri wa miaka 92 katika hospitali ya jeshi katika mji mkuu wa Tunis.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad