Ubutu wa Mastraika Waiangusha Stars Nyumbani...
0
July 29, 2019
UBUTU wa safu ya ushambuliaji ta timu ya taifa, Taifa Stars iliyokuwa chini ya nahodha, John Bocco, umeinyima timu hiyo kupata ushindi nyumbani, licha ya kutawala sehemu kubwa ya pambano lao la kwanza kuwania tiketi ya Fainali za (Chan) za 2020.
Kocha Etienne Ndayiragije aliwaanzisha Bocco, Ayoub Lyanga na Idd Seleman 'Nado' huku akiwaweka benchi Salim Aiyee, Ibrahim Ajibu na Kelvin John aliowaingia kipindi cha pili katika pambano hilo la raundi ya kwanza lililopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Stars ilitawala mpira kwa asilimia 60 za kipindi cha kwanza hasa eneo la kiungo lililokuwa chini ya Jonas Mkude, Abubakar Salum 'Sure Boy' na Hassan Dilunga waliokuwa wakigawa mipira kiufundi wakisaidiwa na krosi za mabeki wa pembeni, Paul Godfrey na Gadiel Michael, lakini washambuliaji walikosa utulivu na kujikuta wakimaliza dakika 90 bila kufunga na Harambee ambao walionekana kuyahitaji matokeo hayo mapema tu.
Matokeo ya jana yanaiweka Stars katika mazingira magumu ya kusonga mbele katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Agosti 4 mjini Nairobi.
Stars itajutia nafasi ambazo ilipata kipindi cha kwanza na kushindwa kuzitumia huku katika kipindi hicho ikifika langoni mwa Kenya mara nne huku Kenya ikifika mara mbili
Read More: Nafasi za Ajira 59 Zilizotangazwa Leo
Harambee Stars ilisubiri hadi dakika ya 13 kufanya shambulizi la kwanza lakini mabeki wa Stars wakiongozwa na Kelvin Yondani na Erasto Nyoni walikuwa makini na kumfanya kipa Juma Kaseja kutosukwasukwa langoni.
Tags