Uingereza Yaionya Iran Baada ya Kuiteka Meli Yenye Bendela Yao

Iran huenda inachagua "njia hatari " ya mwenendo wa " kukiuka sheria na kuvuruga mambo " baada ya maafisa wake kuiteka meli yenye bendera ya Uingereza kwenye eneo la Ghuba, amesema waziri wa mambo ya nje wa uingereza.

Wamiliki wa meli hiyo inayofahamika kama Stena Impero wameshindwa kuwasiliana meli hiyo ambayo ilikuwa imezungukwa na eneo muhimu la Strait of Hormuz.

Serikali ya Uingereza imesema kuwa "inahofu kubwa" juu ya hatua ''zisizokubalika'' za Iran.


Iran imesema kuwa chombo hicho kilikuwa "kinakiuka sheria za kimataifa za vyombo vya majini".


Stena Impero, meli ya yenye bendera ya Uingereza iliyotekwa na Iran kwenye eneo la Ghuba
Meli ya pili ya mafuta ya Uingereza iliyokuwa na bendera ya nchi ya Liberia ,MV Mesdar, pia ilivamiwa na walinzi waliokuwa na silaha lakini baadae Ijumaa iliachiliwa.

Ni nini kilichotokea ?
Stena Impero ilikamatwa na wanajeshi wa Iran al maarufu Iranian Revolutionary Guard siku ya Ijumaa katika eneo muhimu la maji katika Ghuba.

Meli hiyo ya mafuta ilizingirwa na meli nne na helikopta kabla ya kuelekezwa katika eneo la maji la Iran, amesema Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza Jeremy Hunt.

Amesema kuwa "uhusu wa kusafiri majina lazima uimarishwe" na akaonya kuwa itakuwa na " athari mbaya " kama hali haitatatuliwa haraka..

" Hatuangalii hatua za kijeshi ," na kuongeza kuwa: "Tunatafuta njia za kidiplomasia za kutatua hali hii."

Haki miliki ya pichaNORBULK SHIPPING
Image caption
Meli ya Mesdar
Jumamosi Bwana Hunt alituma ujume wa twitter uliosema: " hatua ya jana katika eneo la Ghuba inaonyesha ishara za wasi wasi , Iran inaweza kuwa inmechukua mkondo hatari wa kuyumbisha hali kinyume cha sheria baada ya kumamatwa kwa meli ya mafuta katika eneo la Gibraltar kuelekea Syria."

Shirika la habari linalomilikiwa na taifa la Iran IRNA limesema kuwa meli hiyo ya mafuta ilikamatwa baada ya kugongana na boti la uvuvi na kushindwa kujibu mawasiliano ya meli nyingine ndogo.

Mmiliki wa meli hiyo alisema kuwa ilikuwa inatekeleza kikamilifu masharti na sheria na ilikuwa katika eneo la maji la kimataifa ilipovamiwa na kutekwa.

Imesema kuwa hakuna taarifa za majeruhi miongoni mwa wahudumu wa meli hiyo 23, ambao walikuwa uraia wa mataifa ya India, Urusi, Latvian na Ufilipino.

Iran yakamata meli ya mafuta Ghuba
Iran: Marekani inatusingizia
Msemaji wa serikali ya Uingereza ameiambia BBC kuwa : "tumeshauri meli za mizigo za Uingereza kuwa mbali na eneo la Ghuba kwa muda ."Chombo cha kampuni ya Stena Impero ilikuwa ikisafiri majini ikiwa na bendera ya Uingereza na kusajiliwa London.

''Balozi wetu mjini Tehran anfanya mawasiliano na wizara ya mambo ya kigeni wa Iran kutatua hali hii na tunafanya kazi kwa karibu na washirika wetu wa kimataifa,'' alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad