UN Yataka Uchunguzi Kuhusu Vifo vya Wanafunzi Sudan

Umoja wa mataifa umetoa wito wa kufanyika uchunguzi juu ya mauaji ya watoto watano wa shule katika mkutano nchini Sudan wakati waandamanaji wakiwawekea shinikizo watawala wa kijeshi kuhamisha madaraka kabla ya mazungumzo kuhusiana na kipindi cha mpito nchini humo.

Waandamanaji wamewashutumu wanajeshi wa kikosi cha kutoa msaada wa haraka, kinachoongozwa na jenerali mwenye madaraka makubwa jenerali Mohamed Hamdan Daglo, kwa kuwapiga risasi vijana watano katika mkutano uliofanyika kupinga upungufu wa mikate na mafuta katika mji wa Al-Obeid jana.

Mauaji hayo yanakuja wakati viongozi wa maandamano wanatarajiwa kufanya mazungumzo na baraza la kijeshi leo kuhusiana na vipengee vilivyobakia vya kuanzisha utawala wa kiraia baada ya pande hizo mbili kutia saini makubaliano ya kugawana madaraka mapema mwezi huu.

Wakati huo huo mkuu wa baraza la kijeshi linalotawala Abdel Fattah al-Burhan amenukuliwa akisema kuwa ni lazima kuchukuliwe hatua za uwajibikaji kuhusiana na tukio hilo la kuuwawa kwa vijana hao wa shule.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad