Unaambiwa Mchezaji Roger Milla Alifunga Goli Kombe la Duania Akiwa na Umri wa Miaka 42...Kupewa Tuzo
0
July 28, 2019
Mchezaji wa zamani Cameroon Albert Roger Mooh Milla, Septemba 7 atapewa tuzo na Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kwa kufunga bao akiwa na miaka 42.
Mpaka sasa imeshapita miaka 20 tangu nyota huyo apachk bao hilo kwenye michuano ya Kombe la Dunia.
Bao hilo alifunga kwenye mchezo wa timu yake ya Taifa ya Cameroon dhidi ya Urusi mwaka 1994 na kwa sasa ana umri wa 67
Tuzo hiyo itakuwa ni ya mfungaji mwenye umri mkubwa zaidi katika Kombe la Dunia na itatolewa Septemba 7 nchini Sweden.
Kwenye mchezo huo ambao ulichezwa uwanja wa Stanford nchini Marekani, Cameroon ilipoteza kwa kufungwa mabao 6-1 na timu ya Urusi ambayo nayo ilikuwa imeshatolewa kwenye michuano hiyo mikubwa.
Tags