VIDEO: DPP Asimulia Dhahabu, Fedha zilizotoroshwa Kenya zilivyopatikana


 Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga amesema ushirikiano kati ya ofisi yake na ya DPP wa Kenya imefanikisha kurudishwa Tanzania kwa kilo 35.34 za dhahabu na fedha vilivyotoroshwa kwenda Kenya tangu mwaka 2004.

Akizungumza leo Jumatano Julai 24, 2019  katika hafla fupi ya makabidhiano hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Mganga amesema utaratibu wa kurejeshwa kwa dhahabu hizo ulianza tangu Rais Magufuli alipokuwa mapumzikoni wilayani Chato, mkoani Geita.

“Februari 15, 2018 dhahabu ya kilo 35.34 ilikamatwa katika uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta wakati msafiri mmoja (anamtaja) aliyekuwa akisafiri kwa ndege ya Presission Air kutoka Mwanza alikamatwa,” amesema Mganga.

Amesema baada ya mtuhumiwa huyo kukamatwa Wakurugenzi wa Upelelezi wa Kenya na Tanzania walianza upelelezi, aliongoza timu ya watu 11 kuhakikisha dhahabu hiyo inarejeshwa.

Mbali na timu hiyo, Mganga amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali  (AG), Profesa Adelardus Kilangi aliandika maombi kwenda Kenya kuhakikisha dhahabu hiyo irejeshwe na kutumika kama kielelezo cha kesi.



By Elias Msuya, Mwananchi emsuya@mwananchi.co.tz

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad