Pamoja na kuwa katika hatua za mwisho za kukamilisha mabadiliko ya uendeshaji wa club ya Simba SC kuanza kuendeshwa kwa hisa, wadhamini wa Simba SC wakiongozwa na mzee Hamisi Kilomoni wameendelea kuwa na msimamo wao wa kutotaka kutoa hati za Simba SC kwa muwekezaji wa club hiyo Mohammed Dewji.
Mzee Shaweji Machoyamzungu leo mbele ya waandishi wa habari ameeleza kuungana na mzee Kilomoni kupinga kutoa hati, Shaweji kaeleza na kufika mbali kuwa tatizo sio kuwa na mfumo wa mabadiliko lakini utaratibu unaotumika hakubaliani nao na anaamini ni wakijanjajanja tu.
“Sisi tulipata bahati mbaya naweza kusema hivyo baada ya pale huko nyuma tuliingia katika suala la mali sio mpira bahati nzuri tumekuwa na vijana wetu wa friends of Simba, hii ndio kansa ya Simba afadhali ungekuwa UKIMWI huyu mtu angekufa kwa muda mfupi lakini hii ndio kansa ya Simba SC, kansa hii imetengenezwa na kuandaliwa na Mh Kassim Dewji ameitengeneza vizuri na hivi sasa kila mahali Kassim humuoni”>>>Mzee Shaweji Machoyamzungu