Video: Sakata la Kuvuja kwa Sauti, Nape Afunguka


Kufutia kuvuja na kuenea sauti mbili kwa nyakati tofauti zinazomhusisha akifanya mazungumzo na wanayedaiwa kuwa ni Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Abdulrahman Kinana na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Sengerema William Ngeleja, Mbunge wa Mtama Nape Nnauye amesema suala hilo lina ujinai ndani yake kwa mujibu wa sheria za nchi na kushauri kuviachia vyombo vinavyohusika kushughulikia suala hilo.

Nape ambaye amewahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi katika uongozi wa CCM chini ya Mwenyekiti Rais Mstaafu Jakaya Kikwete amesema hayo wakati akihojiwa na kituo cha runinga cha Azam ambapo amsisitiza ni muhimu watu kuchukua tahadhari katika kujadili suala hili ili wasije kujikuta wanakuwa sehemu ya jinai.

“Vipo vyombo” ambavyo kazi yake ni kushughulikia mambo haya, bila shaka watalishughulikia na wataona undani wake, halafu wataona kama ipo haja ya kuchukua hatua, kwa sababu sheria zipo zinazoliungumzia jambo hili.
“Kwa sababu lina ujinai ndani yake kulizungumzia kwa kina itakuwa ni kuvuruga  vyombo vyenyewe ambavyo vinapaswa kushughulikia,” Nape amesema
“Wanaojadilia waache wajadili lakini pengine wachukue tahadhari lakini waweke akiba ya maneno ili wasije wakawa sehemu ya jinai yenyewe.”

Amesema kwa kuwa vyombo vipo vinasimamia sheria vipo, sheria zinahusu kuhusu masuala hayo pia zipo, basi ni muhimu kuviachia vifanye kazi yao na kuahidi kama kutakuwa na haja ya kulizungumzia suala hilo siku za usoni basi ataweka bayana.

VIDEO


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad