Wachezaji wa Uganda walisusia mazoezi Jumanne katika mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwasbababu ya mzozo wa malipo, kwa mujibu wa shirikisho la soka nchini humo (FUFA).
Ni mzozo wa hivi karibuni kutokea katika mashindnao hayo kufuatia hali kama hiyo kujiri kwa wachezaji wa timu za Zimbabwe, Nigeria na Cameroon.
Timu hiyo ya Cranes iliibuka nafasi ya pili katika kundi lake na inajitayarisha kukabiliana na Senegal katika timu 16 bora Ijumaa.
FUFA linasema wachezaji hao wanajaribu kujadili upya masikizano katika mkataba uliosainiwa kati yao.
Linasema kuwa makubaliano yalifikiwa kabla ya mahsindnao na limetaja malipo ambayo tayari yametolewa kwa wachezaji hao.
"Kufikia tarehe 2 Julai 2019, kila mchezaji alikuwa amepokea hadi $14,600 ... na marupurupu ya ziada ya kila siku na kitita cha ushindi kinachowasubiri," taarifa hiyo imesema
Wachezaji wa Uganda Cranes Wasusia Mazoezi Wakidai malipo
0
July 03, 2019
Tags