Wahamiaji 40 Wauwawa Katika Shambulio Libya

Wahamiaji 40 wauwawa katika shambulio Libya
Karibu wahamiaji 40 wameuwawa katika shambulio la anga jana usiku katika kituo cha kuwashikilia katika kitongoji cha mji mkuu Tripoli shambulio linalohusishwa na mbabe wa kivita nchini Libya Khalifa Haftar, ambaye amekuwa akijaribu kwa miezi mitatu kuukamata mji mkuu Tripoli.

Kiasi watu 70 wamejeruhiwa katika shambulio hilo katika kitongoji cha Tajoura. Msemaji wa huduma za dharura nchini Libya Osama Ali ameliambia shirika la habari la AFP kwamba hiyo ni tathmini wa awali na idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka.

Amesema wahamiaji 120 walikuwa wanashikiliwa katika jengo la kuhifadhi ndege ambalo lilishambuliwa. Miili ya watu ilitapakaa sakafuni katika jengo hilo, ikichanganyika pamoja na vitu walivyokuwa navyo wahamiaji hao pamoja na nguo zilizojaa damu.

 Waokoaji wanatafuta watu walionurusika chini ya kifusi, wakati magari kadhaa ya kubebea wagonjwa yalielekea katika eneo hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad